Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawa
ameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6
ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa
fedha 2023/2024 wa Wizara yake.


Katika hotuba yake ambayo ameshaiwasilisha Bungeni jijini
Dodoma,ameliaambia Bunge kuwa mbali na mambo mengine
yatakayotekelezwa 2023/24, zipo barabara saba zenye jumla ya
urefu wa kilometa elfu 2 na 35.

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo Prof Mbarawa amesema kati
ya fedha hizo Sh Trilioni 1.5 ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi na
Sh Trilioni 2.09 ni kwa ajili ya sekta ya Uchukuzi.

Exit mobile version