In Kitaifa
MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.
Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili, Juni 11, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya Al-Hikma waangalie uwezekano wa   kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships (udhamini) kwa washindi au washiriki, hususan kwa washiriki wa Tanzania.
Waziri Mkuu amewataka wazazi wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Meya wa Temeke, Bw. Abdallah Chaurembo leo  Jumatatu, Juni 12, 2017 afuatane na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bw. Nassib Mmbaga hadi kwenye kiwanja kilichopo eneo la Matumbi na kukagua kama kuna uwezekano wa kuliongeza kwa taasisi ya Al-Hikma na wampe majibu Jumanne kwani limekaa wazi kwa muda mrefu licha ya kuwa walishaliomba na hawakupata majibu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu