Mwanataauluma kutoka nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba amesema kuwa endapo Rais John Magufuli ataendelea na jitihada za kupambana na ufisadi kwa miaka 10, uchumi wa Tanzania utakuwa juu.

In Kitaifa

Mwanataauluma kutoka nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba amesema kuwa endapo Rais John Magufuli ataendelea na jitihada za kupambana na ufisadi kwa miaka 10, uchumi wa Tanzania utakuwa juu.

Profesa Lumumba amesema hayo  kwenye Tamasha la Tisa la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alipokuwa akizungumzia mwanasiasa kuinuka na kuanguka barani Afrika.

Katika maelezo yake, Profesa Lumumba amesema rushwa imeondoa afya barani Afrika, wanasiasa wanapoiacha ikawatawala inawaletea shida.

Aidha amesema kwa kipindi kifupi Rais Magufuli alipoingia madarakani, ameonesha njia kwa wanasiasa wengine barani Afrika, ambao wamekumbatia rushwa na kuwaacha wananchi.

Kwa upande mwingine, amesema kuwa Afrika ni bara zuri na lenye uwezo, ila kilichofanyika kwa miaka 30 iliyopita kumekuwa na viongozi wabinafsi, lakini katika miaka ya sasa wameibuka viongozi wazalendo kama Magufuli, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Yoweri Museveni na wengineo.

Amewataka waafrika wajue watambue kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hivyo ni jambo linalochukua muda mrefu.

 

 

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu