KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL), imepunguza hasara kwa kiasi kikubwa kutoka Sh bilioni 20 hadi kufi kia Sh bilioni 3 kwa mwaka.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi aliyeeleza kuwa katika mpango wao wa muda mfupi ambao ni wa mwaka mmoja, wamefanikiwakupunguza hasara kwa kiasi hicho.
Matindi amesema kufanikiwa huko kumetokana na kufanyika kazi katika baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa ni changamoto ikiwemo ufutaji wa safari, akieleza kuwa awali walikuwa wakifuta safari, lakini kwa sasa hawafuti safari.
Amesema wamejiwekea Mpango Mkakati wa Biashara wa muda mrefu ambao ni wa miaka mitano na kwamba una malengo matatu ikiwemo usalama, kuhakikisha wanatengeneza faida pamoja na kutoa huduma zenye uhakika kwa wateja wao.
