Acacia na Tanzania wakubaliana,Rais apokea taarifa.

Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzani Dr John Pombe Magufuli, leo amepokea taarifa ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya timu ya wataalam aliyoiunda, na timu ya kampuni ya Barrick Gold kuhusu biashara ya ya madini ya dhahabu maarufu kama makinikia.

Akiwasilisha taarifa hiyo mapema leo ikulu jijini Dar es salaam, Antena imemnasa waziri wa katiba na sheria Prof Paramagamba Kabudi, akieleza maeneo ambayo Barrack Gold wamekubaliana na Tanzania.

Kwa upande rais Magufuli amemshukuru mwenyekiti mtendaji wa Barrick kwa utashi wake, na amewashukuru tume za makinikia na timu ya majadiliano ya Tanzania na Bunge.

Amesema anajua huu ni mwanzo wa mazungumzo ulikuwa mgumu, lakini mwisho wa siku anawashukuru kwa kazi nzuri waliyofanya.

 

Exit mobile version