Achimba kaburi ndani ya chumba cha kulala.


Jamaa mmoja wa miaka 25 kutoka kaunti ya Narok nchini
Kenya amewaacha watu vinywa wazi baada ya kuchimba kaburi
katika chumba chake cha kulala.


Kisa hicho cha kushangaza kilipelekea wakazi wa eneo hilo
kufurika nyumbani kwake Geoffrey Lang’at wakitaka kujua ni
kwa nini alichukua hatua kama hiyo.


Kulingana na jamaa huyo kaburi hilo lilikuwa ni lake na
hakuelewa ni kwa nini watu walijihusisha na maisha yake.
Wakati wakazi hao wakizidi kuulizana maswali jamaa huyo
alitoweka ghafla kijijini hapo na haijulikani alikoenda.


Mkewe amesema kuwa Mumewe alimwambia alikuwa akijenga
chumba kingine cha ardhini ndani ya chumba chake cha kulala.
Mwenyekiti wa Nyumba Kumi eneo hilo alithibitisha kisa hicho
na kusema kwamba tayari uchunguzi wa kumsaka Lang’at
umeanza.

Wazee wa mtaa wametangaza mpango wa kufanya tambiko za
kulitakasa boma la jamaa huyo kulingana na mila na tamaduni
za jamii ya Kipsigis.

Exit mobile version