Adam Malima afutiwa kesi,Kaka na Dereva wake waongea.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuachia huru Naibu Waziri wa zamani Adam Malima kutokana na kesi ya kushambulia iliyokuwa ikimkabili.

Adam Malima ambae juzi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, yeye na Dereva wake ndio walikua wanakabiliwa na kesi hiyo ambapo Mkurugenzi wa mashtaka amesema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Antena imemnasa dereva wake Ramadha Mohamed pamoja na kaka yake Malima, mara baada ya kesi hiyo kufutwana walikuwa na haya ya kuongea.

 

Exit mobile version