Chama cha Allience for Democratic Change ADC, kimelaani kushambuliwa kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tumdu Lissu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Hassan Doyo amesema matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea hapa nchini likiwemo la kushambuliwa mbunge Tundu Lissu, hayakubaliki hata kidogo.
Aidha chama hicho kimetoa ushauri kwa serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalam juu ya mataukio hayo.
