Afisa mtendaji awataka Wananchi kuendelea na majukumu yao ya kujipatia kipato.

In Kitaifa

Afisa mtendaji wa kata ya Kisongo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Bw. Brighton Mwandii amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea na majukumu yao ya kujipatia kipato wakati wanaendelea kupambana na kujikinga na virusu vya corona


Akizungumza na vyombo vya habari habari mtendaji huyo amesema kuwa, kata ya Kisongo ni mojawapo ya kata iliyopo wilaya ya Arumeru kati ya kata 27 ambayo imekuwa ikiendelea na shughuli mbalbali za kiuchumi ili kuweza kulijenga taifa
Amesema kwa kipindi hiki wananchi wa kata hiyo wanaendelea na swala la kilimo na ufugaji ili kuweza kuendelea kuzalisha nafaka mbalimbali amapo hii itasaidia kuondoa changamoto ukosekanaji wa vyakula hapa nchini


Mtendaji huyo amewahasa wakulima na wafugaji kilimo cha muda mfupi ili kuweza kuzalisha kwa wingi na piwa wajasiriamali kuendelea na biashara zao ndogondogo ili waweze kuangalia familia zao na kuweza kujikwambua kimaisha
Amesema kuwa, kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona wananchi wanaendelea kupewa elimu namna ya kuchukua taadhari ya kujikinga kwa kunawa mikono na maji yanayotiritika na sabuni, kukaa umbali wa futi mbili, kuepuka mikusanyiko isiyo ya ulazima, kuvaa barakoa, na kuosha mikono na vitakasamikono.


Mh.Brighton amewataka wazazi kukaa karibu na watoto waa hasa kwa kipindi hiki wakiwa majumbani na kuwapa elimu ya afya ya uzazi kutokana na changamoto ya watoto wengi kupata mimba zisizotarajiwa na kuharibu maisha yao ya badae
Hata hivyo amewataka vija wa kike na kiume kuacha kudanganyana na kujikita kwenye vitendo viovu na badala yake wamuombe Mungu na kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao na hatimaye kulijenga taifa

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu