Afisa wa afya wa Yemen amesema zaidi ya watu 96,000 wameambukizwa maradhi ya kipindupindu katika mlipuko uliosababisha vifo vya watu wapatao 746 tokea mwezi Aprili.
Nasser al-Argaly, katibu wa afya katika serikali inayoongozwa na uasi mjini Sanaa, amesema mlipuko huo wa kipindupindu umetokana na kampeni ya mashambulizi ya miaka miwili inayongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa jamii ya Houthi.
Mapigano hayo yameharibu miundombinu na kusababisha kuwepo uhaba wa dawa.
Maafisa wa afya nchini Yemeni wamesema ndege zilizokuwa zimebeba misaada ya kiutu ya tani 50 za dawa za maradhi ya kipindupindu kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, ziliwasili katika mji wa kusini wa Aden, ambao unadhibitiwa na vikosi vya serikali.
