Afisa wa serikali ya Kenya amesema wafanyakazi 4 wa misaada nchini Kenya, wamepoteza maisha baada ya gari yao kukanyaga bomu karibu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab, katika kaunti iliyoko mashariki mwa Garissa.
Mohamud Saleh mratibu wa mkoa wa kaskazini mashariki, amesema gari hilo ni mali ya shirika la African Development Solutions.
Amesema inadhaniwa kuwa bomu hilo lilikuwa limetegeshwa na kikundi cha siasa kali ya Al-Shabab, ambacho kiko nchi ya jirani ya Somalia.
Inaelezwa kuwa zauidi ya watu 34 wamepoteza maisha mpaka sasa wakiwemo maafisa wa polisi 20, katika milipuko nchini humo katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.
