Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi George Simbachawene, amewahakikishia wabunge ahadi zote alizoziahidi Rais John Magufuli wakati wa kampeni zitatekelezwa.
Simbachawene ametoa kauli hiyo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai Chadema Freemon Mbowe.
Mbowe alitaka kujua ni lini serikali itatoa bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita tano za lami, ambazo Rais aliahidi wakati wa kampeni.
Akijibu swali hilo Simbachawene amesema ahadi zote alizotoa Rais wakati wa kampeni, zitatekelezwa ndani ya miaka mitano kama alivyoahidi.
