Ajali ya barabarani yaua watu 27 nchini Kenya.

Polisi nchini Kenya wanasema kiasi ya watu 27 wameuawa hii leo baada ya basi la abiria kugongana na lori nchini humo.

Polisi wanasema tukio hilo limetokea katika barabara kuu inayounganisha miji miwili mikubwa nchini humo ya Nairobi na bandari ya Mombasa.

Leonard Kimaiyo ambaye ni mkuu wa polisi katika eneo la Kambu kwenye kaunti ya Makueni amesema basi hilo lilikuwa likielekea Mombasa na lori lilikuwa liielekea upande mwingine wakati ajali hiyo ilipotokea.

Ajali za barabarani zinaua takribani watu 3,000 nchini Kenya kila mwaka.

Vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vimeongezeka nchini humo katika miaka ya karibuni licha ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa ikiwa ni pamoja na kutozwa fani kali na vizuizi vya barabarani.

Exit mobile version