Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki , amesema ameamua kuondoka serikalini baada ya utumishi wa muda mrefu ,na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki.
Aidha Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dk John Pombe Magufuli, kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa.
Sadiki amesema hayo jana wakati wa mahojiano maalum na kuhusu sababu zilizochangia ,kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema Sababu nyingine kubwa ni kuhofia afya yake kutomudu kasi ya rais Magufuli, kwani alifanywa upasuaji mwaka 2012 na 2014 nchini India ingawa hakutaka kuweka wazi maradhi yaliyokuwa yakimkabili.
Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 ,alipoteuliwa na Rais Magufuli, amesema siyo vibaya, kwa kiongozi kujitathmini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua.
Kwa upande wake Afisa Habari wa mkoa huo, Shabani Pazi amesema mkoa umeshtushwa na uamuzi wa mkuu wa mkoa kwani hawakuwa wameuratajia kwani tangu amefika mkoani humo watumishi walioko chini yake walianza kumuelewa na kwenda na kasi yake
