Kamati ya nidhamu inatarajia kumhoji beki wa Majimaji, Juma Salamba.
Salamba atahojiwa kutokana na tuhuma ya kumtwanga kiwiko hadi kuzimia, kiungo wa Yanga, Emmanuel Martin.
Salamba atapanda katika “kizimba” cha kamati ya nidhamu leo tayari kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo katika mechi iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
