ALIYOSEMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIWA NJIANI KUELEKEA DAR ES SALAAM JULAI 30, 2020

In Kitaifa

Ilibidi niende na ndege Dar es Salaam lakini nimepita hii barabara makusudi nione hali yake, hii barabara imeharibika, km 90 zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii barabara

Barabara hii ya Lindi-Dar es salaam imeharibika sana. Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri.

Nimetoka Masasi kulikua na madeni yamebaki ya wakulima wa korosho, Tumetoa TZS Bilioni 20, hakuna mkulima yoyote wa korosho atakaedai, tumemaliza madeni yote,TZS Bilioni 20 zimetolewa wiki iliyopita na bado watu wanaendelea kulipwa.

Tumeshalipa zaidi ya TZS Bilioni 800 kwaajili ya korosho, tumemaliza na hii TZS Bilioni 20 zilizobaki. Tuendelee kushikamana na Serikali yetu na tuendelee kuchapa kazi. Mtwara na Lindi ya sasa sio kama ya kipindi cha nyuma, zinapendeza, zinafurahisha

Kazi aliyoifanya Mkapa ameifanya kwa nguvu zote na mimi nawaomba wananchi wa kusini tumuenzi Mkapa kwa kuchapa kazi. Tuna eneo zuri mno, Ufuta unakubali, Korosho zinakubali, mahindi yanakubali na mifugo inakubali. Tuchape kazi na tupendane kwa ajili ya taifa letu. Kero ya barabara hii nimeibeba.

Tunatuma fedha za Bodi ya Mfuko wa Barabara [Road Fund] na tunatuma fedha za Halmashauri haiwezekani hakuna stendi eneo hili. Uchaguzi unakuja, tujipange vizuri na tuchague wawakilishi ambao tutawabana, ambao watatuwakilisha vizuri

Kwa mujibu wa Sheria ya Barabara, barabara ikishakua ya lami inapata 100% ya ukarabati [Maintanance]. Fedha za Bodi ya Mfuko wa Barabara [Road Fund] sijui zinakwenda wapi, Serikali haijalala, hili nawahakikishia nitalishughulikia mwenyewe. Naomba muiamini Serikali.

Wananchi wa Somanga tuendelee kuchapa kazi. Wakulima wote wenye korosho halali wamelipwa na bado wanaendelea kulipwa.

Naichangia Shule ya Msingi Somanga TZS Milioni 5. OCD wa hapa hakikisha hizi fedha zinaenda benki na zinapelekwa katika hiyo shule, mkazitumie kweli nitakuja nifuatilie lakini TZS 100,000 ibaki kwa huyu mtoto

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu