Amani Golugwa amesema kuwa hawaridhiki na mazingira ya madiwani wao saba kujivua nafasi zao za madaraka.

In Kitaifa

Katibu wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema kuwa hawaridhiki na mazingira ya madiwani wao saba kujivua nafasi zao za madaraka.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa sakata hilo wameamua kulifikisha kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili iweze kutafutiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa haoni sababu yeyote ya msingi ya viongozi hao kujivua nafasi zao ndio maana wamefikia hatua hiyo ya kulifikisha jambo hilo mbele ya vyombo hivyo ili viweze kulichunguza kiundani zaidi.

Hata hivyo, amewataka wafuasi wa Chama hicho kutotafuta mchawi bali wafukuze wasaliti waliomo ndani ili waweze kukijenga na kuimarisha utendaji kazi wake katika kutoa upinzani uliokuwa imara.

Hivi karibuni madiwani saba wamejivua uanachama wa chama hicho katika kata za Abureni, Ngabobo, Muriet, Legaruki, Makiba, Maroroni na mwingine ni wa diwani wa viti maalumu kutoka chama hicho.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu