Amjeruhi mpenzi wake kwa risasi wakiwa hotelini…


Polisi mkoani Geita inamshikilia mfanyabiashara Bw.Salum
Othman mkazi wa jijini Mwanza kwa tuhuma za kumjeruhi kwa
kumpiga risasi kwa bastola mpenzi wake Happyness Israel
wakiwa nyumba ya kulala wageni majira ya saa nne asubuhi
katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo mtaa wa Nyamalembo,kata
Mtakuja mjini Geita pamoja na kumjeruhi Meneja wa hoteli
hiyo Ndugu John Maftaa alipotaka kutoa msaada wa kumdhibiti
mtuhumiwa Salum Othman.
Taarifa hiyo imethibitishwa hapa mtaa wa mastory na Kamanda
wa Polisi Geita Mponjoli Mwabulambo huku Chanzo cha tukio
hilo kinadaiwa ni wivu wa mapenzi.


Mkurugenzi wa Hoteli Ndugu Paulo Limo yeye pia ameelezea
namna tukio lilivyotekea hotelini hapo.

Naye Kaimu Mganga mfawidhi katika hosptali ya rufaa Mkoani
Geita Dk,Shaban Massawe yeye amethibitisha kuwapokea
majeruhi wawili na pia ameelezea namna alivyowapokea
sambamba na hali zao.

Exit mobile version