Andengenye akabidhiwa ofisi ya Mkoa Kigoma.

.

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma Brig Jeneral Mstaafu Emanuel Maganga, amemkabidhi ofisi mkuu mpya wa mkoa huo CP Thobiasi E.M Andengenye,aliyeteuliwa hivi karibuni na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Brig Maganga,ameeleza namna alivyoukuta mkoa huo wakati anaingia na kumtaka mkuu huyo mpya kuendeleza pale alipoishia ili kupandisha uchumi wa mkoa wa Kigoma.

Kwa upande wake mkuu huyo Mpya wa mkoa wa Kigoma CP Thobiasi E.M Andengebye, amezungumza kwa mara ya kwanza na kushukuru kwa kupokelea vyema katika mkoa huo lakini pia akawataka watendaji wa serikali katika mkoa huo kuepuka rushwa ili wananchi wa mkoa huo wapate haki kwa usawa.

Exit mobile version