Antonio Conte na Jose Mourinho watupiana vijembe.

In Kimataifa, Michezo

Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte, amemwambia kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwamba aangalie timu yake na aache kufuatilia masuala ya klabu ya Chelsea.

Kauli ya Antonio Conte inakuja baada ya Jose Mourinho kudai kwamba, kuna makocha ambao wachezaji wao wakipata maejeraha huwa wanapiga sana kelele kauli ambayo ilionekana kama kijembe kwa Conte.

Conte amesema hawezi kuhatarisha afya za wachezaji wake, na kwa kuwa wameumia kidogo atawaacha nje ya uwanja hadi pale watakapokuwa fiti kuanza kucheza.

Chelsea imeambulia alama moja tu katika michezo yao mitatu iliyopita katika msimu huu, na Jumamosi hii wataikabili Watford huku Ngolo Kante,Victor Moses,Tiomoue Bakayoko na David Luiz wakiwa mashakani kuukosa mchezo huu.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu