Arsenal kumenyana na Tottenham, debi ya London.

The Gunners pia itamkagua beki Shkrodan Mustafi na Danny Welbeck ambao wamerudi katika mazoezi huku Alexandre Lacazzette akitarajiwa kucheza.

Harry Kane , Dele Alli na Harry Winks wote wanatarajiwa kushiriki licha ya kukosa kuichezea Uingereza kutokana na matatizo ya majeraha.

Kipa Hugo Hloris, ambaye hakucheza katika mechi ya ushindi dhidi ya Crystal Palace kutokana na jereha la nyonga pia huenda akashiriki.

Kipa wa ziada Michel Vorm alirudi katika mazoezi siku ya Alhamisi na atakaguliwa, lakini Toby Alderweireld ana jeraha baya la nyonga na huenda beki huyo akasalia nje hadi baada ya sikukuu ya Krisimasi.

Exit mobile version