Arsenal wakataa £50m kutoka Man City.

In Kimataifa, Michezo

Arsenal wamekataa dau ya £50m kutoka kwa wapinzani wao Ligi ya Premia Manchester City, ambao wanataka kumchukua mshambuliaji nyota kutoka Chile Alexis Sanchez.

Sanchez 28 alifungia Arsenal mabao 24 Ligi ya Premia msimu uliopita, lakini mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Arsenal wamekataa majaribio yoyote ya kutaka kumchukua Sanchez kufikia sasa, na wangefurahia sana iwapo Raheem Sterling atakuwa kwenye sehemu ya mkataba wake kuhamia City.

Meneja wa City Pep Guardiola inadaiwa hata hivyo kwamba anataka kumnunua Sanchez 28 moja kwa moja.

Hata hivyo hatua ya kumnunua inaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City.

Sterling 22 anayechezea timu ya taifa ya England, amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu.

Lakini hatahakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco.

Sanchez bado hajatia saini mkataba mpya Emirates.

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili.

Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m, na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu