Arsene Wenger asema ‘alisita’ kutia saini mkataba mpya Arsenal.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ”alisita” wakati wa kutia saini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita kwa sababu hakuwa na uhakika kwamba ”angeweza kuiongoza klabu hiyo.”

Wenger alikubali mkataba wa miaka miwili mwezi Mei, mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Kwenye runinga moja nchini Ufaransa ya Telefoot, alisema alikuwa na ”sababu za kibinafsi” kutokana na uamuzi uliochelewa wa kuongeza muda wake wa miaka 21 na klabu hiyo.

Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano katika Ligi ya Premia msimu uliopita, ikiwa ni mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nambari nne tangu Wenger alipojiunga na klabu hiyo mwaka 1996.

Arsenal walianza michuano ya msimu huu ya Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa nyumbani wa magoli 4-3 dhidi ya Leicester,kabla kupoteza kwa Stoke kwa goli 1-0 na Liverpool 4-0.

Exit mobile version