Arsene Wenger: Sanchez na Ozil hawaondoki ng’o.

In Kimataifa, Michezo

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji Alexis Sanchez na kiungo wa kati Mesut Ozil wataichezea Arsenal baada ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari hadi pale ”kitu kisiochoaminika kitakapofanyika”.

Kandarasi ya wachezaji hao wawili inakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa iwapo anahisi watasalia, Wenger alijibu: Ndio kabisa.

Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa Jack Wilshere pia anataka kusalia na klabu hiyo ya ligi ya Uingereza.

Wenger aliongezea: Nitampigania asalie hapa kwa sababu ni mchezaji mzuri.

Mchezaji wa Uingereza Wilshere mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akikumbwa na majeraha tangu alipoingia Arsenal 2008 huku akihudumu msimu wa mwaka 2016-17 kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth.

Hatahivyo hajaanzishwa msimu huu.

Wote, Sanchez mwenye umri wa miaka 28 na Ozil mwenye umri wa miaka 29 ni viungo muhimu wa Wenger.

Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye aliwasili kutoka Barcelona 2014 amefunga mabao 56 katika mechi 113, huku Ozil ambaye ni raia wa Ujerumani akitoa usaidizi wa mabao 45 tangu alipojiunga 2013 ikiwa ni zaidi mchezaji yeyote yule.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu