Imeelezwa kuwa idadi ya Watanzania wanaojisaidia vichakani
imepungua kutoka asilimia 5.7 mwaka 2017,hadi asilimia 1.4
Desemba 2021.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,
wakati akitaja mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya
Nyumba ni Choo kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka
mitano ya kampeni hiyo nchini.
Amesema sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika
baadae mwaka huu itatoa takwimu halisi ni kwa kiasi gani
Watanzania wamefanikiwa katika kuwekeza katika kuwa na
vyoo bora,na kuyataja baadhi ya maeneo yaliyofanya vizuri
katika kampeni hiyo.