Asilimia 13.4 tu ndio wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

In Kitaifa

Imeelezwa kuwa hali ya usajili na takwimu za matukio ya vizazi,vifo ndoa na talaka nchini hairidhishi kutokana na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, zinaonyesha kuwa asilimia 13.4 ndio wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma  na Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa PALAMAGAMBA KABUDI  wakati alipokuwa akifungua kikao cha wadau kuhusu usanifu mpango wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na ukusanyaji wa takwimu.

Profes KABUDI amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Serikali imeamua kufanya maboresho ya Mfumo wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali kutokana na hali ya usajili nchini kutokuwa ya kuridhisha.

Aidha amebainisha kuwa Idadi hiyo ni ndogo na ni kiashiria kuwa Serikali haina taarifa za idadi kubwa ya wananchi ambapo licha ya kuwepo kwa takwimu hizo hivyo kukosa kumbukumbu.

Pia Profesa KABUDI amesema kuwa maboresho hayo yanatekelezwa kupitia mkakati wa Kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na kwamba  usajili wa matukio muhimu ndio mfumo mama katika nchi yoyote.

Naye Profesa HAMISI DIHENGA ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakala wa Usajili,udhamini na ufilisi (RITA)amewataka wananchi wote kujitokeza kwaajili ya kujisali ili wapate vyeti vya kuzaliwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu