Askari atiwa mbaroni kwa mauaji ya Mkewe.

In Kitaifa

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Daniel Warioba anatuhumiwa kumuua mkewe ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani, Joyce Ismail (35) na kisha kutaka kujiua. Polisi inamshikilia askari huyo mwenye umri wa miaka 43 kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo ni la Desemaba 4, mwaka huu saa saa 10 alfajiri eneo la Janga Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

“Mtuhumiwa alimuua mkewe Joyce Ismail (35) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kisha na yeye kusadikiwa kunywa sumu akitaka kujiua bila ya mafanikio,” alisema Kamanda Nyigesa.

Alisema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na mtuhumiwa anashikilia akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi kwa matibabu zaidi chini ya ulinzi.

Katika hatua nyingine, Polisi imetoa taarifa ya tukio lingine la mauaji linalomhusisha mfanyakazi wa shambani anayetuhumiwa kumuua mwajiri wake, Halima Pwipwi (50) kwa kumkata kwa mapanga mwilini.

Kamanda Nyigesa alisema mauaji hayo yamefanyika juzi usiku katika Kijiji cha Mpaji Wilaya ya Kipolisi Chalinze na kwamba mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda uhalifu huo.

Alisema kijana huyo ambaye jina halikufahamika, alifanya mauaji hayo ambayo hata hivyo chanzo chake hakijfahamika na polisi wanaendelea na msako kumtafuta kijana huyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Aidha, Polisi inawatafuta watu wanaotuhumiwa kuchoma moto nyumba ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Matwipili, Issa Mwakilasi (40) na kumsababishia maumivu mwilini. Thamani ya mali zilizoungua ni Sh 35,000.

“Mwalimu baada ya kuona moto unawaka kwenye nyumba anayoishi ambayo ni mali ya shule, aliona moto huo kupitia dirishani na kuanza jitihada za kuuzima moto huo na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Kamanda Nyigesa na kwamba wahusika wanatafutwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu