Baba wa watoto wa Kourtney kardshian, aachana na mpenzi wake Sophia Richie

Baba wa watoto wa Kourtney kardshian, Scott Disick ameachana na mpenzi wake Sophia
Richie alianza uhusiano wake 2017, hii inafuatia skendo mbali mbali, ambapo mwaka 2018
wawili hawa walitengena baada ya Scott disick kumcheat mwanadada huyu, lakini waliweza
kurudiana miezi kadhaa baadae, na skendo ya hivi karibuni ni ile ya kuondoka kwenye sober
house baada ya mmoja wa wafanyakazi kumpiga picha, na kuisambaza kwa maneno
kwamba scott amerudi kwenye ulevi na madawa ambapo aliyakananusha hayo na kuahidi
kuwafungulia kesi kwani wamevujisha siri za mgonjwa wao.


Lakini leo Scott amethibitisha uvumi wa kuachana na mpenzi wake huyu Sophia Richie
ambae alikua ni msaada mkubwa katika kumsaidia kuacha madawa na ulevi wa kupindukia,
sababu ya kuachana hasa inasemekana kwamba wawili hawa katika kipindi cha lockdown
kila mmoja amekuwa akiji karantini mwenyewe hivyo distance huenda ikachangia lakini pia
inasemekana kwamba Kourtney Kardashian pia ana nafasi kubwa ya kucheza katika hili
kwani hajafanya uhusiano huu uwe kwa Amani.

Exit mobile version