Babalevo kuminyana na Zitto Ubunge

Msanii Babalevo ambaye ni diwani aliyemaliza muda wake katika kata ya Mwanga Kaskazini Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia chama cha ACT wazalendo, amesema sasa anakwenda kugombea ubunge.

Msanii wa Bongo Fleva na Diwani mstaafu, Babalevo amesema ni muda sasa wa kuwania ubunge na atakwenda kugombea katika jimbo la Kigoma Mjini.

”Baada ya hapa naondoka naelekea Kigoma kwa wananchi wangu nakwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini kama Mh Zitto hatagombea lakini akigombea nitaenda jimbo jingine”, amesema.

Babalevo amehudumu kama diwani wa Mwanga Kaskazini kwa miaka mitano lakini pia amewahi kutumia kifongo jela, ambapo mwenyewe anasema jela ilimfundisha mambo mengi ikiwemo kumjua Mungu.

Kwa upande mwingine Babalevo amesema akipata kiinua mgongo chake cha Mil 20 au zaidi basi Mil 10 atazirudisha kwa wananchi wake.

Exit mobile version