Hakika ukishakuwa Msanii mkubwa wa Kimataifa wewe ni Tajiri asiyemithilika.
Kama ilivyo kawaida, Mtandao wa YouTube wenyewe tu huwa unampa mwenye account Dollar 3000 kwa kila Views Million 1 kwenye YouTube Channel ya Muhusika.
Sasa kwanini nasema ukishakuwa Msanii Mkubwa umeula, Mwanamuziki Enrique Iglesias, anasherehekea Wimbo wake wa Bailando aliowashirikisha Descemer Bueno na Gente De Zona kufikisha Watazamaji (Views) zaidi ya bilioni 2 kwenye mtandao huo wa Youtube tangu umewekwa 11 Apr 2014.

August 2015, ilipata views zake za kwanza bilioni moja na kuwa wimbo wa kwanza wenye lugha ya Spanish kufikia Watazamaji hao.
Enrique Iglesias amesherehekea kwa kuwashukuru Mashabiki wake kwa Kuandika kwenye nstagram, “Thank you to all my fans! I love you guys!”
Hii Inatupa Picha ya Haraka haraka kwamba kwakuwa Views Million 1 anapewa Dollar 3000, Basi Enrique ameingiza Kiasi cha Dollar Million 6 ambazo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trillion 18 (18,000,000,000)
UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO HIYO HAPA CHINI
