Matamshi yake yanajiri kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Baraza hilo siku ya Jumatatu kwa pamoja lilishutumu jaribio la kombora la masafa marefu lililotekelezwa na Korea Kaskazini na kuonya kuhusu vikwazo vipya.
Korea kaskazini inesema kuwa kombora hilo lililofanyiwa majaribio ni jipya na lina uwezo wa kubeba kichwa cha kinyuklia.
Lilisafiri urefu wa kilomita 700 na kwenda juu kilomita 2000 kabla ya kuanguka magharibi mwa bahari ya Japan.
Hatahivyo Korea Kusini ilishindwa kubaini habari hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa faragha wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne , bi Harley aliyaonya mataifa yanayounga mkono Korea Kaskazini kuwacha kauli hiyo la sivyo yaone cha mtema kuni.
Washington alisema, inaunga mkono mazungumzo na Pyongyang iwapo taifa hilo litasitisha majaribio ya makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia
