Bara la Afrika limedhimisha miaka 54 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika OAU, ambao siku hizi unafahamika kama AU.

In Kimataifa

Bara la Afrika limedhimisha miaka 54 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika OAU, ambao siku hizi unafahamika kama AU.

Tarehe 25 mwezi Mei  Mwaka 1963, viongozi wa mataifa ya Afrika walikutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia na kuunda Umoja wa kuwaunganisha kwa lengo kubwa la kupambana na ukoloni na kumaliza ubaguzi dhidi ya waafrika.

Wakati huo, mataifa 32 yalitia saini mkataba wa kuanzisha Umoja huo, huku malengo mengine yakiwa ni pamoja na kuwa na msimamo mmoja kuhusu maswala yanayoliathiri bara la Afrika.

Muungano huo pia ulilenga kusaidia mataifa ya Afrika kusaidia kuimarisha maswala ya kisiasa, kijamii na kisiasa na kwa lengo la kujenga bara lenye Umoja na mshikamano.

Suala lingine lililokuwa ni kuhimiza amani, usalama na udhabiti wa bara la Afrika.

Hata hivyo, ilipofika mwaka 2001, muungano huo ulibadilishwa kuwa OAU na kupewa jina lingine la AU-Umoja wa Afrika.

Viongozi wa sasa wamekuja na malengo mbalibali kujaribu kuimarisha maisha ya Waafrika wakiwa na lengo la muda mrefu kuwa ifikapo mwaka 2063, itakuwa imemaliza umasikini na kuwa bara thabiti.

Kufikia mwaka 2020, Umoja wa Afrika unataka kuwepo kwa amani na usalama katika mataifa yote na silaha kuwekwa chini hasa katika mataifa yanayoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama kama Somalia, Libya, Sudan Kusini na  Mashariki mwa DRC miongoni mwa mengine.

Mataifa 55 yanayounda Umoja huo baada ya kuongezeka kwa Sudan Kusini iliyojitenga na Sudan mwaka 2011 na kurejeshwa kwa Morocco mwanzoni mwa mwaka 2017, yanataka kuwa na uwezo na ushawishi wa kiuchumi na kisiasa.

Miaka 54, baada ya Waafrika kuja pamoja, umasikini, magonjwa, vita, miundo mbinu mibaya na kuendelea kupata misaada kutoka Mataifa ya Magharibi ni baadhi ya changamoto ambazo bado inaendelea kukabiliana nazo.

Kitu pekee ambacho bara la Afrika limefanikiwa kwa muda huo wote ni kupambana na kumaliza  ukoloni, ambao hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema umeanza kurejea kwa njia ya misaada ya kifedha huku mataifa yakiendelea yakichukua rasilimali za mataifa ya Afrika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu