Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuanzisha ofisi ya kupambana na ugaidi, ili kuratibu juhudi zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuanzisha ofisi ya kupambana na ugaidi, ili kuratibu juhudi zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ni mageuzi makubwa ya kwanza ya kitaasisi yaliyofanywa katika Umoja wa Mataifa tangu Bw. Antonio Guterres aanze kuongoza umoja huo.

Bw. Guterres siku hiyo alitoa taarifa kupitia msemaji wake, akikaribisha kupitishwa kwa azimio hilo, na kusema anatarajia kuwa mageuzi hayo yanaweza kuhimiza juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuzuia mgogoro na kuhimiza maendeleo na amani ya kudumu.

Exit mobile version