Baraza la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), wametakiwa kuungana na kuweka mipango mikakati ya nguvu ili kuhakikisha wanaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Kauli hiyo imetolewa na  Mama REGINA  LOWASSA  wakati akizungumza na wanawake wa baraza hilo katika mkutano wao wa kikao cha ndani na kikao cha kazi ambacho kimefanyika mjini Dodoma.

Pia amesema juhudi za akina mama wa Chadema zilizofanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilikuwa na nguvu kubwa hivyo kuna kila sababu ya kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha akina mama wanagombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa BAWACHA HALIMA MDEE ,amewataka akina mama kuhakikisha wanafanya kazi kwa ujasiri na kuhakikisha wanapata nafasi mbalimbali katika ngazi za maamuzi.

MDEE  amewaamasisha wabunge wote wa Viti Maalum, kuhakikisha wanatafuta majimbo na kutafuta nafasi mbalimbali za maamuzi badala ya kuwa na hofu na kujiona kana kwamba zipo nafasi mbalimbali ambazo zinafaa kugombewa na na wanaume na siyo wanawake.

Exit mobile version