Baraza maalum linalochunguza tuhuma za Urusi launda jopo kuu.

In Kimataifa

Baraza maalum linalochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana linaarifiwa kuunda jopo kuu.

Gazeti la The Wall Street Journal linasema jopo hilo kuu la Robert Mueller limeanza kazi katika wiki za hivi karibuni na limewasilisha agizo la kukusanya ushahidi kuhusu mkutano wa Juni mwaka jana kati ya mwanawe rais Trump na wakili mmoja wa Urusi.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa uchunguzi wa Robert Mueller’umechukua hatua ya kwanza kuelekea ufunguzi wa mashtaka ya uhalifu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters , jopo hilo la mahakama limewaita mashahidi kuzungumzia juu ya mkutano wa mwezi Juni mwaka 2016 baina ya mtoto wa kiume wa rais Donald Trump .. Trump Jr na wakili wa Urusi.

Rais Trump anapinga madai yoyote kwamba maafisa wake walikula njama na serikali ya Urusi ili kumshinda Bi Hillary Clinton katika uchaguzi wa urais.

Nchini Marekani , jopo kubwa la mahakama huundwa kwa ajili ya kuchunguza ikiwa ushahidi uliopo ni wa kutosha kiasi cha kufungua kesi ya mashtaka ya uhalifu.

Jopo kubwa la mahakama hata hivyo haliamui juu ya kutokuwepo na hatia wala uwezekano mtu kuwa na hatia.

Taarifa ya kwamba jopo kubwa la mahakama limekuwa likikutana mjini Washington DC, na kwamba linachunguza mkutano wa June 2016 baina ya Donald Trump Jr na raia wa Urusi, ni wazi kwamba uchunguzi sasa unaelekezwa kwa wandani wa rais.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu