Benki za wakulima na taasisi za kifedha nchini zimetakiwa kuwakopesha wakulima ili wanunue zana za kilimo kwa lengo la kuboresha kilimo ili kiwe na tija.

In Kitaifa

Benki za wakulima na taasisi za kifedha nchini zimetakiwa kuwakopesha wakulima ili wanunue zana za kilimo kwa lengo la kuboresha kilimo ili kiwe na tija.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea kampuni ya kuunganisha matrekta ya Ursus kutoka Ujerumani, ambako pia alitembelea Kituo cha Uwekezaji cha EPZA, na kiwanda cha ulainishaji vyuma cha Kamal Industrial Estate kilichopo wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yake mkoani Pwani ya kutembelea viwanda.

Waziri Mkuu alisema ili dhana ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati lazima vyanzo vya kuinua uchumi viwekewe mazingira mazuri.

Aidha, alisema serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje na kuwataka Watanzania wenye marafiki wa nje wenye uwezo wa kuanzisha viwanda wawaite ili wawekeze.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema mradi huo ni endelevu wa kuunganisha matreka kwa lengo la kuboresha kilimo ili kiwe na tija na kuinua uchumi wa wananchi.

Mwijage alisema hadi sasa kiwanda hicho tayari kimeunganisha matrekta 2,400 ambayo yatasambazwa nchi nzima ambapo kutaanzishwa vituo vinane kwa ajili ya kuwafikia wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema kwa sasa Mkoa wa Pwani umefanikiwa kuwa na viwanda vikubwa 84 kati ya viwanda 393 nchini; na kwamba tatizo ni upungufu wa umeme wa uhakika ambapo mkoa unahitaji megawati 60 ambapo kwa sasa mkoa unapata megawati 48.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu