Bibi harusi akatazwa kutabasamu kwenye harusi yake.

 

Ukiuliza kila mwanamke alieolewa atakwambia namna siku ya harusi ni siku ya furaha kwa mwanamke.

Huko Tajiskistan nchi iliyo bara la Asia, mwanadada Hudoidodova mwenye miaka 22 amelazimika kutotabasamu na kutomwangalia mume wake machoni siku ya harusi yake kutokana na tamaduni zao kutoruhusu.

Ukitabasamu inaonyesha mlijuana kabla ya ndoa jambo ambalo hairuhusiwi, pia bibi harusi akifurahi inaonyesha amefurahi kuacha familia yake na kumfata mume wake.

Alipoulizwa kama aliolewa kwa kulazimishwa alisema hapana na alifurahia kupata mwanamme anaemruhusu kufanya kazi baada ya kuolewa tofauti na wanaume wengine waliomtaka zamani.

Raisi wa nchi hiyo Emomail Rahman, aliona Asrovov hana mke na kuwaamuru wataalamu wa kuwatafutia watu wachumba, wamtafutie ndipo wakampata mwanamke huyo aitwaye Hudoidi.

Exit mobile version