Biden : Trump anatuma ujumbe wa vitisho

In Kimataifa

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amelaani kitendo cha Donald Trump kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais, amesema kuwa ‘anatuma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani’.

Bwana Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa bwana Trump alikuwa anajua kuwa hasingeshinda na kila kitu kilionekana wazi , kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la Georgia, na bwana Biden alipata ushindi katika jimbo hilo.

Bwana Trump alifungua kesi ya madai ya wizi wa kura.

Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.

Bwana Biden amepata ushindi wa kura za umma kwa zaidi ya milioni 5.9 .

Ushindi wake katika kura za wajumbe ambazo zinaweza kuthibitisha nani anakuwa rais aliweza kukadiriwa kupata kura 306 mpaka 232.

Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden alisema rais anatuma ujumbe wa kutisha… kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi, na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu