Bilionea atoa kampuni yake kupambana na Mabadiliko ya hali ya hewa

In Kimataifa
Bilionea mwanzilishi kampuni ya mavazi Patagonia anasema ametoa kampuni yake kwa wakfu wa uhisani .

Yvon Chouinard alisema kuwa chini ya muundo mpya wa umiliki, faida yoyote ambayo haijawekezwa tena katika kuendesha biashara itaenda kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hii itafikia karibu $100bn ($86bn) kwa mwaka, alidai, kulingana na hali ya kampuni.

Patagonia inauza mavazi ya kupanda mlima na mavazi mengine ya shughuli za nje katika zaidi ya nchi 10.

Ilianzishwa mwaka 1973, mapato yake yalikuwa $1.5bn mwaka huu, huku thamani ya Bw Chouinard inadhaniwa kuwa $1,2bn.

“Licha ya ukubwa wake, rasilimali za Dunia sio nyingi, na ni wazi kuwa tumevuka mipaka yake,” mjasiriamali huyo alisema juu ya uamuzi wake wa kuacha umiliki.

“Badala ya kutoa thamani kutoka kwa asili na kuibadilisha kuwa utajiri, tunatumia utajiri ambao Patagonia inaunda kulinda chanzo.”

Kampuni hiyo ya California ilikuwa tayari ikitoa 1% ya faida yake ya kila mwaka kwa wanaharakati wa ngazi ya chini na kujitolea kwa shughuli endelevu. Lakini katika barua ya wazi kwa wateja, mfanyabiashara huyo anayeonekana kusitasita alisema alitaka kufanya zaidi.

Alisema awali alikuwa amefikiria kuuza Patagonia na kutoa pesa kwa mashirika ya hisani, au kuipeleka kampuni hiyo kwa umma.

Lakini alisema chaguzi zote mbili zingemaanisha kuacha udhibiti wa biashara. “Hata makampuni ya umma yenye nia njema yana shinikizo kubwa la kutengeneza faida ya muda mfupi kwa gharama ya uhai na uwajibikaji wa muda mrefu,” alisema.

Badala yake, familia ya Chouinard, ambayo imekuwa inamiliki kampunim hiyo imeihamisha kwa vyombo viwili vipya. Patagonia Purpose Trust, inayoongozwa na familia, inasalia kuwa mbia mkuu wa kampuni lakini itamiliki tu 2% ya hisa zake zote, Bw Chouinard alisema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu