Bilionea ‘Hushpuppi’akamatwa kwa utapeli

Bilionea Ramon Olorunwa Abbass Maarufu kama ‘Hushpuppi’
kupitia mtandao wa Instagram mwenye thamani ya Dolla za
kimarekani $20M na aliyejitambulisha kama real estate agent,
amekamatwa na polisi wa Dubai, akiwa na wengine kumi na mbili kwa
kosa la kutapeli watu kupitia mtandao, utakatishaji wa pesa zaidi ya
Bilioni 1.6 pesa za Dubai na kutumia vitambulisho vya watu .
‘Hushpuppi’ mwenye umaarufu mkubwa sana mtandaoni ambapo
anafollowers zaidi ya 2.4M ambapo ukurasa wake hujaa picha
zikionyesha maisha ya kifahari, akindesha magari makubwa na hata
kuwa na gari customized kutoka aRolls Royce, pia anamiliki Private
Jet na latest Range Rover ,


Hushpuppi mwenye uraia wa Nigeria, alikua akita uangalizi wa polisi
kwa miezi kadhaa kwani walikua wanamhisi kuwa ni muhalifu,
ambapo waliweza kupata ushahidi kwamba yeye na wenzake
wamekua wakifungua website feki zinazofanana na kurasa za benki
na makampuni mbali mbali, na kuelekeza watu kutuma pesa, lakini
walitumia vitambulisho vya watu tofauti tofauti ili kujipatia fedha,
lakini pia waligundua kuwa yeye na wenzake hao walihack email ya
kampuni moja ya malipo huko Dubai na kuelekeza pesa hizo kwao.
Wakati askari wameenda kuwatia mbaroni washtakiwa hawa walikuta
ushahidi wa mpango wa kutakatisha fedha za Dubai Bilioni 1.6, pia
walikua pesa taslim milioni 150, computer 21, smartphone 47,
memorycard 15, hard disk tano zenye mafile 119,580 ya taarifa za
watu zaidi ya millioni mbili waliowahi kutapeliwa, biashara 81 feki
ambazo zinafanya kazi kwenye nchi 18 kutapeli watu, email 800,000
za makampuni ya watu,na ushahidi wa kuiba zaidi ya Dirhan Bilion4,
na pia wameweka kuzuizini magari yake zaidi ya 12 yenye thamani
ya zaidi ya dola millioni moja za kimarekani ambazo ni sawa na dolla
millioni 220 za kimarekani kwa gari moja..

Exit mobile version