Bodi ya korosho Tanzania yaongeza vituo vya ugawaji pembejeo.

In Kitaifa

Bodi ya korosho Tanzania imeongeza vituo vya ugawaji pembejeo ili kuharakisha usambazaji na kuhakikisha kila mkulima anapata pembejeo kwa wakati katika kudhibiti kuenea kwa magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao la korosho.

Akitolea ufafanuzi tuhuma za ucheleweshwaji wa madawa na viuatilifu Mwanasheria na Katibu wa Bodi hiyo, Ugumba Kilasa amesema kuwa bado wapo ndani ya wakati kwa kuwa matumizi ya viuatilifu huanza mara tu korosho zinapotoa maua mwezi Juni.

Amesema kuwa kufikia Agosti 20, 2017 usambazaji wa pembejeo kwa wakulima wote kwa msimu mpya utakuwa umekamilika kwani tani zilizobaki kukamilisha usambazaji kwa wakulima wote tayari zimeingia bandarini na zipo katika taratibu za kutolewa ili kusambazwa.

Hata hivyo,  amewaonya wale wanaotoa maneno ya kuwavunja moyo wakulima wa zao hilo kuhusu kusambazwa kwa madawa na viuatilifu kwambi si huduma ya bure na kusema kwamba serikali imeamua kutoa madawa hayo kwa wakulima bure na kila mtu atapata kulingana na mgawo wa madawa hayo

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu