Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini HESLB, imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo.
Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha.
Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo AbdulRazaq Badru, amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4.
Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa elfu 49 mia 2 na 82 lakini ni elfu 15 mia 4 na 73 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao
