Borussia Dortmund Wapata ajali na Basi lao

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani jana Jumanne ilipata majonzi baada ya kutokea kwa mlipuko katika basi lao lililokuwa linasafirisha wachezaji wake kuelekea uwanjani.

Dortmund ilitakiwa kucheza na As Monaco ya Ufaransa katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya (Uefa). Mechi hiyo ilighairishwa kutokana na mlipuko huo uliosababisha mchezaji mmoja wa timu hiyo Marc Bartra kuumia.

Hata hivyo mchezaji huyo ameshafanyiwa upasuaji wa mkono wake usiku wa April 11 baada ya kuvunjika mfupa kutokana na tukio hilo

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC News umeripoti kuwa shambulizi hilo linahusishwa na kikundi cha Islamic State kutoka Syria. na mchezaji Marc Bartra ndio mchezaji pekee wa Dortmund aliyeumia katika tukio hilo.

Exit mobile version