Bunge kupiga kura ya kutokua na imani na Mugabe.

In Kimataifa, Siasa

Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang’anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg’oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 “kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba”.

Vingozi wa kijeshi ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni.

Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.

Jumapili , licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBA 7, 2023

Manchester United na Newcastle United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 20, ambaye mkataba wake unamalizika Juni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu