Bunge la Nepal limemchagua mwanasiasa mkongwe Sher Bahadur Deuba, kama waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.
Hii ni kwa mara ya nne Deuba kuwa waziri mkuu wa taifa hilo la milima ya Himalaya.
Ni kiongozi wa 10 wa Nepal katika miaka 11, na alichaguliwa bila ya kupingwa katika uchaguzi uliofanyika bungeni Jumanne uiliyopita.
Deuba ataongoza serikali ya mseto na chama Moaist Center, kinachoongozwa na mtangulizi wake, aliyekuwa mkuu wa vita vya msituni Pushpa Kamal Dahal.
