Bunge lapiga marufuku masuala ya usalama wa Taifa kujadiliwa Bungeni.

Bunge limepiga marufuku masuala ya Usalama wa taifa kujadiliwa ndani ya chombo hicho, isipokuwa kama mbunge anaweza kuwasilisha hoja mahususi.
Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ametoa uamuzi huo jana, wakati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Angelina Malembeka alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka wa fedha wa 2017/18.
Katika kuchangia mjadala huo Malembeka alisema Idara ya Usalama wa Taifa inapaswa kuanza kuwahoji wabunge, walioeleza kuwa wana orodha ya wabunge 11 wanaotarajiwa kutekwa nyara na idara hiyo.

Exit mobile version