Bunge latangaza nafasi za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka CHADEMA.

In Kitaifa

BUNGE limetangaza kuwa, uchaguzi mdogo wa kupata wawakilishi wawili wa nafasi ya ubunge kwa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ,kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sasa utafanyika Mei 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Bunge ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Thomas Kashilillah, uteuzi wa wagombea utafanyika Mei 3.

Aidha amesema watakaopigiwa kura na kuchaguliwa katika uchaguzi huo wataungana na wengine saba, sita wakiwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ,ambao walishinda katika uchaguzi wa Aprili 4, mwaka huu.

 

Siku hiyo, Chadema licha ya kuweka wagombea wao Lawrence Masha na Ezekiah Wenje, kura zao hazikutosha hivyo kukosa sifa za kuchaguliwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu