Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.
Hoja hiyo imetolewa Jana bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.
Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.
Exit mobile version