Bunge limepitisha sheria mpya ambayo sasa itatambua haki na dhamana ya serikali katika makinikia, ambayo itakuwa ni marufuku kuchenjuliwa nje ya nchi.
Sheria hiyo inaeleza kuwa serikali itashiriki kwa asilimia kuanzia 16 hadi 50 katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchejuaji madini, na ununuzi wa hisa katika kampuni ya uchimbaji madini.
Aidha Wakala wa Ukaguzi wa Madini TMAA umefutwa rasmi, na sasa kunaanzishwa Kamisheni ya Madini.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesema kufutwa kwa TMAA, kunatokana na majukumu yake yaliyokuwa yakitekelezwa na wakala huyo, kuhamishiwa kwa Kamisheni ya Madini.
Kuanzia sasa umiliki wa leseni mbalimbali zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Madini,hautahamishwa kabla haujafanyiwa uendelezaji katika kitalu husika.
