Bunge Misri limekubali kurejesha visiwa viwili vilivyoko bahari ya Sham kwa Saudi Arabia, chini ya makubaliano yenye utata ya uchoraji mpaka.
Visiwa hivyo visivokaliwa vya Tiran na Sanfir vilimilikiwa na Saudi Arabia hadi miaka ya 1950, wakati Riyadh ilipoiomba Cairo kuvilinda dhidi ya uwezekano wa kushambuliwa na Israel.
Na kweli Israel ilishambulia na kuviteka visiwa hivyo mwaka 1967, lakini baadae ilivirejesha kwa Misri kama sehemu ya makubaliano ya Camp David yaliofikiwa mwaka 1979.
Saudi Arabia imekuwa ikiomba kurudishiwa visiwa hivyo mara kwa mara. Lakini mpaka hivi karubuni, maafisa wa Misri walikuwa wanasita kukubalia maombo hayo.
Wapinzani wa serikali wanamtuhumu rais Abdel-Fattah al-Sisi kwa kuuza ardhi ya nchi kwa wadhamini wake.
Athari za kisheria za uamuzi huo hazikuwa bayana, ingawa visiwa hivyo vinaweza kutumiwa kwa maslahi ya pamoja ya usalama ya mataifa hayo.
